THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI) - EPISODE 05

 

Nilijikuta nikiogopa sana, pale nilipoona funza wengi wamejaa katika kitanda changu. Baada ya sekunde kadhaa nilisikia jogoo wakiwika huku ndege nao wakitoa sauti kuashiria kwamba kumekucha. Wakati nikiendelea kutetemeka kwa woga nilishangaa kuona wale funza wakijikusanya kisha wakageuka na kuwa mfupa wa simba. Nilijaribu kuutupa ule mfupa wa simba ilishindikana. Ghafla nilimsikia mama mdogo akisema wewe ni muongo. Kijana wangu Kelvin hawezi kutembea sasa hilo duka kalifungua saa ngapi?.


Mama ninakuapia mimi nimemwona sasa hivi kabisa Kelvin akiwa dukani kwake na akiwa amezungukwa na wateja. Hebu subiri kwanza nimuite alisema mama mdogo huku akiingia chumbani kwa Kelvin. 

"Wewe Kelvin" 

"Kelvin kijana wangu." 

Naam mama mdogo. Umesikia hebu ingia huku ndani umtizame Kelvin sasa sijui umemwona Kelvin yupi kule dukani?. Baada ya yule kijana kuingia chumbani. Yule kijana aliguna kisha akasema hapana hii haikubaliki hata kidogo. Kabla Kelvin hajauliza sababu iliyomfanya yule kijana kuingia kwenye chumba chake. Ghafla yule kijana alikimbia huku akisema 

"Kelvin ni jini." 

"Jamani Kelvin ni jini" 

"Kelvin sio mtu wa kawaida ".

Yule kijana alikimbia mpaka mbagala rangi tatu ambako Kelvin alikuwa akiuza mchele na maharage. Jamani Kelvin ni jini. Kelvin ni nusu mtu nusu jini. Mbona sikuelewi tatizo nini?. Aliuliza mfanyabiashara anayeitwa Tizo. Yule kijana alianza kuelezea jinsi alivyomkuta Kelvin yupo dukani akiwa anauza mchele na maharage lakini pia Kelvin huyohuyo yupo nyumbani kwao. Wewe uko sawa kweli nahisi umetumia "catalyst ya ubongo"(bangi), hivi inawezekana vipi Kelvin mmoja awe sehemu mbili tofauti. 

"Wewe ni muongo."

"Umetumia catalyst ya ubongo"

Mfanyabiashara Tizo aliongezea kwa kusema catalyst ya ubongo inaumiza sana vijana. Tizama sasa umetumia catalyst ya ubongo sasa hivi unaongea vitu vya ovyo ovyo kabisa. Hebu kaa kimya sitaki kusikia upuuzi wako. Baadhi ya wafanyabiashara wengine walisogea kusikiliza lakini Tizo aliwambia msipoteze muda wenu huyo ameshatumia catalyst ya ubongo. Usishangae akatuambia yuko Ziwa Victoria anaogelea. Wakati Tizo anamaliza kuongea vile ghafla walishangaa kumwona Kelvin akishuka kwenye bajaji. Yule kijana alisema si mlikuwa mnakataa tizama sasa Kelvin huyo anashuka kwenye bajaji halafu Kelvin huyohuyo yupo dukani anauza mchele na Maharage. Wafanyabiashara  walisema kumbe ni kweli sijui Kelvin ni mzimu. Hapa hapatufai walisema huku wakianza kukimbia ovyo.


Baada ya Kelvin kushuka kwenye bajaji, waliongozana na mama yake mdogo mpaka dukani kwa Kelvin. Kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka kujua ni Kelvin yupi anayeuza dukani?. Mama mdogo alisema lazima tutaujua ukweli, hebu sogea kwenye duka lako. Mmmh!!, ni kweli duka limefunguliwa sasa sijui nani anauza, wakati Kelvini akimaliza kuongea alipigwa na butwaa kwa kile alichokiona dukani mwake, si yeye tu hata mama mdogo wake alipatwa na mshangao mkubwa kwa kile alichokiona dukani kwa Kelvin.


****

Angelina hakuwa na amani, alibaki akiwaza juu ya kutafutwa na polisi akiwa katika dimbwi la mawazo akajikuta akilitaja jina la Dickson. Muda huohuo askari walifika na kumuweka chini ya ulinzi. Mkurugenzi wa hospitali ya MFALME SULEIMAN, alibaki mdomo wazi kila alipojaribu kuuliza aliambiwa na askari kwamba Angelina ni muuaji aliyetoroka gerezani. Mkurugenzi wa hospitali ya MFALME SULEIMAN, alijikuta kwenye hatia hii ni baada ya kuishi na muuaji. Kwa kuwa alikuwa na pesa za kutosha aliamua kutoa rushwa ili awe huru. Askari walipokea ile rushwa kisha wakamweka Angelina kwenye difenda.


Baada ya kufika kituo cha polisi, Angelina alianza kupokea mateso makali huku akiulizwa aseme sababu iliyopelekea awakate wenzake titi la kushoto. Unajifanya jeuri alisema Afande mmoja huku akichukua prize nakuanza kuvuta kucha za kwenye vidole vya mikono. Angelina aliugulia maumivu makali sana, lakini alikuwa akisema  hajui kitu chochote kuhusu wafungwa wenzake kukatwa titi la kushoto. 



ITAENDELEA.......... 

Je, Kelvin ameona kitu gani dukani kwake.

Upande mwingine Angelina anapata mateso makali lakini anasema hajui ni mtu gani aliyewakata wafungwa wenzake titi la kushoto. Ili kuyajua yote yatakayojili usikose kusoma sehemu ya 6 ya hadithi yako tamu ya THE DEVIL TONGUE (ULIMI WA SHETANI). 

Post a Comment

0 Comments